Wednesday, December 20, 2006

Nas featuring Quan-Just A Moment

Kwa ndugu, jamaa, na marafiki wetu wote..letz take a moment for them..we all miss them.. alwayz gonna b hot song!!!

Friday, December 15, 2006

Tatizo Letu Sisi Wabongo:

Hivi jiulize kuna vitu vingapi vibovu au dili(backdoor issues) unazozijua kuhusu serikali yetu?..Jiulize tena, kama unavijua umevipata wapi?...Magazeti, Tv or kijiweni?..mengi ni kwenye vijiwe, bar, mara chache sana kwenye magazeti. Tatizo letu sisi wabongo ni waoga wa Changes. Wabongo kazi yao ni kuongea na kulalamika tu kwamba huyu kafanya hivi, huyu kaiba hivi, hii si halali kabisa, lakini hatuwezi kusimama na ku-demand changes for the sake of ourselves, our family, and nchi yetu kwa ujumla. Wabongo tuna-umimi sana, nishibe mimi kwanza then nimuulize mwenzangu kama amekula!. Wangapi walijua kwamba TANESCO ilinunuliwa na watu wanne tu?..mmoja wao ni mtoto wa aliyekuwa Raisi(mnajua jina lake)? Wengi tu walijua lakini walifanyanya nini? waliongea, wakalalamika, wakaandamana siku moja ikaisha..na mjadala ukafungwa. Mnakumbuka watu wangapi walikosa benefits zao baada ya hao filauni wanne kuchukua TANESCO?....imagine wewe umefanya kazi miaka 30 na siku moja all your benefits zinachukuliwa?..ndio yaliyotokea kwa wengi tu..wengi tu wao ni wazazi wetu au wa rafiki zetu, pengine ndugu zetu lakini hatukuwa na nguvu ya kusema liliko mioyoni mwetu! Na Nani hajui kuhusu mkataba wa IPTL?? wabongo walifanya nini kwani?....kimyaaa...

Wabongo wanajua makapuni mangapi yamechukuliwa na wageni kwa hasara( i.e. NBC etc) na watu kupoteza kazi lakini wamekaa kimya(..kuongea kwenye bar au kijiweni ni sawa na kukaa kimya). Hii kasumba iliyowekwa na Chama tawala(sijui chama gani) inabidi ibadilishwe. Chama Tawala wanajua kwamba wabongo kazi yao ni kuongea na hawajali..thatz why they can do anything mbele ya macho yetu bila uoga na aibu na wanajua wananchi hawatafanya kitu. Mwezi tu uliyopita, zilipitishwa budget za ki#@$% na wengi tu walijua lakini nini kimefanyika?
Kwanini tunalalamika sisi maskini, au ohh serikali haifanyi kazi yake wakati hatuna hata uwezo wa kuikosoa hiyo serikali na viongozi wetu hatuna?

Itz time to stand up, sio kuchukua silaha( ukifika muda wake..why not), bali kuongea, kutoa maoni yako, kutoa sauti yako ili isikike. Muda wa kukaa kimya umepita, paza sauti upate mahitaji ya lazima ya binadamu( i.e maji, umeme, na chakula). Muda wa kujua wala rushwa, viongozi wachafu, wasio na huruma ya kutumikia wananchi wake na kukaa kimya umepitwa na wakati. Unajua kuna watu wangapi hapo Bongo land wana hela za kumwaga na watu wanajua za wizi.sa kwanini ukae kimya? unajua viongozi wa ngapi wamekopa mamilioni ya hela na bado hawajalipa, sasa kwanini ukae kimya?

Hatuwezi kusaidiwa bila sisi kujisaidiwa kwanza! Wakati ndio huu, Kwanini wabongo tulipe umeme ghali kusini mwa bara la afrika wakati si ni maskini wa kutupwa?..Kwanini hatuwezi kuwa na umeme bila matatizo after more than 40 years of independence? ..Simama toa dukuduku lako, maoni yako......

tatizo la hivi karibuni la kampuni ya Richmond. Hivi kuna kiongozi serikalini ambae anajua right and wrong?.nyie shenzi serikali mmeiba mmetosheka au wateva lakini kutuwekea kampuni feki..c'mon guys..yaani serikali inaona watu wote zaidi ya millioni 30 ni wajinga au?..this is the main reason ambayo nilikuwa naongelea kwenye paragraphs za mwanzo..serikali inajua sisi wabongo hatuwezi kufanya chochote..inajua sisis ni wapumbavu au tunakaakimya tu zaidi ya kupiga stori but we got no balls to stand up and kulazimisha mtu ajiuzulu. Ushawahi kuona wapi au kusiki lini since unakua kwamba kuna kiongozi bongo amejiuzulu kutokana na pressure za wananchi..mi nafikiri ukitaka kazi rahisi duniani kote ni kuwa mbunge, waziri au raisi wa Tanzania! trust me..hizo kazi hazina malengo( goals), no planning, hamana pressure kabisa yaani.

Yeah yeah raisi anajitahidi na blah blah blah..najua nitapingwa na wengi lakini still he hasnt done anything that suprise us at all.. sanasana tunaona viongozi waislamu wanazidi kuongezeka katika madaraka serikali. Mimi sina budget ya raisi lakini nadhani huyu raisi wa sasa ametumia hela zaidi ya raisi mwingine yeyote wa Tz kwa kusafiri tu katika kipindi kifupi. Kama una common sense, utatumiaje hela zote kusafiri nje all the time wakati nchi yako haina umeme almost 22 hrs a day?..hamna maji safi karibu mji mzima, shule za sekondari hazitoshi, madawati hamna, dawa hospitali hazitoshi, na mambo mengi tu yanayotia huruma.

Unaweza kupiga picha Tz itakuwa wapi baada ya miaka 20? Kama una umri wa kutosha au wazee wetu walipiga picha enzi hizo ( i.e kama 1970s or 1980s) kwamba 2006/2007 ) nchi itakuwa haina umeme?..yaaani badala ya nchi kwenda mbele, Tanzania inarudi nyuma. wabongo inabidi tuache mambo ya kuongea tu, itz time to stand up for the next generation ( i.e.nafikiri changes generation yetu ni mbinde..vihwa vilivyo serikali ni vigumu sana).

kwa wale walio bongo, wanafurahi kupata bidhaa sasa hivi za nje ovyo ovyo lakini hawajui kwamba wanau bidhaa za ndani ya nchi. Ma-supermarket kibaoa mazuri yanafunguliwa na yana vitu vizuri sana yaani na bei yake ni ghali sana yaani. lakini anagalia percentage ya wanaoenda kufanya shopping huko. Most ni wadosi, wazungu au mbantu ambaye ana hela na hao ni asilimia chahe tu ya watanzania wote. Je wale asilimia nyingi ya wabongo wa kawaida wako wapi katika hili? wanafaidika nini? Tukisema hii ni kumtumikia mwenye hela sana ni uongo?

Ni kweli kabisa serikali kidogo kuna nidhamu ambayo imelewa na JK lakini hiyo nidhamu itadumu wakati hao wafanyakazi wanalipwa hela ndogo bado? Bdo kuna mambo ya niweke mimi nitakulisha au unakumbka nilishokufanyia zamani. Favors bongo bado zipo hata kama wewe huzisikii ila sinakuwa kwenye category tofauti na ya zamani. Kwa kweli nchi yetu inanuka viongozi wasio na maadili, nidhamu, creativity, leadership skills, and upeo.

Tuna watu wengi tu wenye vipaji mbalimbali nje ya nchi. Ushawahi kujiuliza kwanini hawarudi bongo kusaidia nchi yao?..utasaidiaje kitu ambacho hakiwezi kujisaidia chenyewe?.. we all agreed that u alwayz learn something mtoni au popote ulipo nje ya nchi ulipo kuanzia responsibility and accountability. Mi nadhani sio tu kulaumu watu wa nje kwamba hawataki kurudi bongo kusaidia kujenga nchi. wabongo wote duniani, popote pale, we all have the same problem, issue: Viongozi wetu/serikali yetu isiyo na mwelekeo na ambao hawajali maslahi ya wananchi bali ya kwao. Hivi unaweza kweli kujenga nchi bila kuwa na long term plan?..

Kwa wale ambo mnaona kukosa umeme almost all day na kukosa maji safi ni haki..sawa.. poleni wenzangu na mimi ambao mna fikra kama zangu, itz time now to stand up against the gov. Tuonganishe nguvu zetu za hoja ili sauti zetu zisikii..sauti ya watu ina nguvu zaidi ya sauti yako peke yako! Lets make our gov works for us and our families not for themselves!!

Hayo ni Maoni tu..no personal feelings! Mbongo mwenzio!

Thursday, December 14, 2006

birdman ft lil wayne - stuntin like my daddy (dirty)

KJ stuntin like his daddy!!!

Wednesday, December 13, 2006

Avant ft Lil Wayne - You Know What

wow..damn..luuuv this song.. u know wat..u know how..am gonna u know what..this is the Shit..Avant break down this shit!!..Favourite R&B of the year
Lil Wayne - Way of Life

Damn..dd u see those ppl shinin on it..life iz good if everyday is like that! enjoy..it..flyin any weather
Lil Wayne - Shine (old Hit)

yeah..still we gonna make it!! We gonna shine..lol

Sunday, December 03, 2006

Si Matani

New SI matani Music! Itz a narrative clip of song called
"siamini" produced and written by Kolumba and Akili AKA Mtaalamu
Esther Baxter

Felllas..we both wish..damn..shorty will u b mine?